PICHA: MTANANGE WA SIMBA NA AZAM FC ULIVYOKUWA CHAMAZI

Kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Yahya Zayed akienda chini mbele ya mabeki wa Simba, Method Mwanjali na Ally Shomary katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka sare 0-0

Winga wa Simba, Shiza Kichuya akijivuta kupiga krosi pembeni ya kiungo wa Azam, Himid Mao 

Mshambuliaji wa Azam, Mohammed Yahya akienda chini kwenye boksi baada ya kukwatuliwa na beki wa Simba, Salim Mbonde 

Kiungo wa Simba, Said Nemla akipiga shuti jana Uwanja wa Azam Complex

Mshambuliaji wa Simba, John Bocco akibinuka tik-tak kakati ya mabeki wa Azam, Aggrey Morris (kushoto) na Yakubu Mohammed (kulia)

Winga wa Azam, Ennock Atta Agyei akimtoka beki wa Simba, Erasto Nyoni 

Mshambuliaji wa Azam FC, Mbaraka Yussuf akimtoka Shiza Kichuya wa Simba

Ramadhani Singano 'Messi' wa Azam akimuacha chini Method Mwanjali wa Simba

Kikosi cha Azam FC katika mchezo wa jana

Kikosi cha Simba SC katika mchezo wa jana

Maoni