Viongozi wa dini waingilia umri wa Rais

Baraza hilo linalojumuisha wakuu saba wa madhehebu makubwa ya dini nchini humo limesema katika taarifa yao ya pamoja kwamba watu waruhusiwe kuamua hatma yao.
Wamependekeza mjadala wa taifa uandaliwe kuhusu ukomo wa umri wa Rais na baadaye ifanyike kura ya maoni na kutoa wito kwa Rais Yoweri Museveni kuonesha ukomavu wa kiutawala katika suala hilo.
Hivi karibuni wabunge wa chama tawala cha National Resistance Movement, NRM walipitisha uamuzi wa kuondolewa ukomo wa umri wa miaka 75 uliowekwa katika Katiba.
Endapo marekebisho hayo yatapitishwa Bungeni, itakuwa na maana kwamba Rais Museveni mwenye umri wa miaka 73 sasa ataweza kugombea uchaguzi ujao mwaka 2021 akiwa na umri wa miaka 77. Mwaka 2005, katiba ilifanyiwa marekebisho ukaondolewa ukomo wa mihula miwili ya miaka mitano kila mmoja.

Maoni