AJALIMAKETE

Gari la Kampuni ya Japanese aina ya Mitsubishi Rosa yenye namba za usajili T437CLT limepata ajali baada ya kufeli breki eneo la mpaka wa kijiji cha Luvulunge na Iwawa Makete
Ajali hiyo imetokea jumapili hii majira ya saa 7 mchana, Gari hilo linalofanya safari zake Mbeya Ikonda-Makete lilikuwa na abiria zaidi ya 20 ambao wengi wao wamepata majeraha madogomadogo na kukimbizwa hospitali ya wilaya ya makete kwa matibabu.
Chanzo cha ajali hiyo kwa Mujibu wa Dereva Noah Sanga amesema ni kufeli kwa breki za gari hiyo ikiwa Kwenye mteremko mkali na kuacha barabara kisha kuelekea mtoni na kuvuka mto
Ikumbukwe ni mwezi mmoja umepita tangu kutokea kwa ajali ikihusisha basi la kampuni hiyo maeneo ya mlima Lwamadovela kata ya lupalilo wilayani makete iliyosababisha kifo cha abiria mmoja na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Maoni