Ali Kiba: Najisikia Vizuri Watu Maarufu Kupenda Kazi Zangu na Nina Haki Kupendwa na Mange Kimambi

Alikiba ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake wa 'Seduce me' amefunguka na kusema kuwa Tanzania kila mtu ana haki na uhuru wake hivyo hata yeye anajisikia vizuri kuona watu maarufu wanapenda kazi zake na kudai ana haki ya kupendwa na Mange Kimambi

Alikiba amedai kuwa Mange Kimambi ni moja kati ya mashabiki zake na kusema anashukuru sana kuona anapenda kazi zake na kumpa nguvu katika kazi zake hizo kwa kutoa 'support'.
"Ni kama shabiki wangu na 'appreciate' anapenda muziki wangu kwa sababu mimi namuheshimu kila mtu ambaye kwa namna moja au nyingine anani 'support' kwenye kazi zangu lakini pia kutokana na uhuru hivyo kila mtu ana haki na vilevile mimi nina haki ya kupendwa na mtu yoyote yule, hivyo nina haki ya kupendwa na Mange Kimambi pia" alisema Alikiba

Mbali na hilo Alikiba alisema anajisikia vizuri kuona muziki wake unazidi kufika mbali zaidi duniani na kuendelea kufanya vizuri nyumbani Tanzania na Afrika Mashariki kiujumla.
"Najisikia furaha zaidi pale napoona watu wanaojulikana na maarufu nao wanafurahi na muziki wangu na si kusikia muziki tu bali ni mashabiki wangu pia, hivyo kwangu mimi ni raha sana, nawapenda sana mashabiki zangu wote duniani kwani nyinyi mnanipa furaha na amani" alisema Alikiba 

Maoni