BABA AUA MWANAE KISA KUOLEWA NA KUKATISHA MASOMO YAKE

Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Masesa Sesaguli mkazi wa kitongoji cha Mwakakongoro kijiji cha Butini kata ya Itwangi katika wilaya ya Shinyanga anadaiwa kumuua kwa kumpiga fimbo mtoto wake wa kike Nshoma Masesa (16) mwanafunzi wa shule ya Sekondari Buhongwa iliyoko mkoani Mwanza.
Wanaeleza kuwa mwanafunzi huyo ameacha shule mwaka huu kisha kutoroshwa na mwanaume huko Kahama ili akaolewe ndipo mzazi wake (Masesa Sesaguli) akaamua kumfuata wilayani Kahama alikoolewa kisha kumwadhibu kwa kumchapa mpaka umauti kumfika.
Taarifa za tukio hilo ni kuwa baba amefanya unyama huo octoba mosi mwaka huu na kutokomea kusiko julikana.

Maoni