Faida za chai na kahawa kiafya:

1. Kahawa au chai inaweza kukuongezea nguvu mwilini
Kikombe cha chai na kahawa kinaweza kukufanya usijisikie mchovu na kukuongezea nguvu mwilini.
Hii ni kwa sababu ndani yake kuna kuna kichangamsho (stimulant) kiitwacho kafeina. Kafeina ni aina mojawapo ya dawa za kulevya kundi la vichangamsho (stimulant drugs) ambayo ndiyo stimu inayotumiwa zaidi kuliko kitu kingine chochote cha kuongeza stimu duniani.
Ukinywa tu chai au kahawa yako mara moja inaingia kwenye mkondo wa damu na kutokea hapo inaenda mpaka kwenye ubongo ambako hukutana na transmita nyurolojia iitwayo ADENOSINE.
Linapotokea hilo kiasi cha transmitanyurolojia nyingine ‘norepinephrine’ na ‘dopamine’ huongezeka na kukupelekea kujisikia vizuri zaidi na kukupunguzia uchovu.
Tafiti nyingi zinathibitisha kaffeina huimarisha kazi kadhaa za ubongo. Kazi hizo ni pamoja na zile zinahusiana na masuala ya kumbukumbu, tabia, nguvu, uharaka wa kujibu mambo nk.
2. Husaidia kuchoma mafuta mwilini
Kama ulikuwa hujuwi kaffeina ni kiungo mhimu kwenye dawa nyingi za kupunguza uzito au mafuta mwilini za viwandani ingawa wakati mwingine inaweza isitwaje kwenye vifungashio vya hizo dawa.
Kaffeina ni moja ya viinilishe vya asili ambavyo vimethibitishwa kuwa vinasaidia kuchoma mafuta mwilini.
Tafiti kadhaa zinaonyesha kaffeina inaweza kuuongezea nguvu mfumo wa mmeng;enyo wa chakula kwa asilimia 3 mpaka 11.
Tafiti nyingine zinasema kaffeina inaweza kuongeza kazi za uchomaji mafuta mwilini kwa asilimia hadi 10 kwa watu wenye uzito na unene uliozidi huku ikiongeza kuchoma mafuta kwa asilimia mpaka 29 kwa watu wembamba au wenye uzito mdogo.
Hata hivyo kazi hii ya kuchoma mafuta huwa inapungua nguvu zake kadri mtu anavyozidi kuitumia chai au kahawa kwa muda mrefu zaidi au kwa wingi zaidi.
3. Kuna viinilishe kadhaa vizuri kwenye chai na kahawa
Kahawa au chai ya rangi ni zaidi ya yale maji meusi. Kuna viinilishe kadhaa vizuri kwa mwili wa binadamu. Viinilishe hivyo ni pamoja na vitamini B5, manganizi, potasiamu, magnesiamu nk
Ingawa hiyo siyo ishu sana lakini kuna watu wanakunywa vikombe viwili mpaka vine vya kahawa kwa siku hivyo kwao viinilishe hivi kunakuwa na uhakika wanavipata.
4. Kafeina inaweza kukuepusha kisukari aina ya pili
Kisukari aina ya pili ni janga la kidunia na ni ugonjwa unatesa watu zaidi ya milioni 300 dunia nzima.
Kisukari aina ya pili ni wakati ambapo insulini inakuwa huru (insulin-independent) au inapatikana lakini kongosho haliitoi na hivyo dawa (kemikali) lazima itumike kulilazimisha kongosho kutoa insulini.
Kwa kiasi fulani wanywaji wa chai na kahawa wanapata kinga ya kutokupata kisukari aina hii ya pili.
Tafiti zinaonyesha kuwa watu wanaokunywa chai ya rangi na kahawa wana asilimia mpaka 67 za kutokupata kisukari aina hii.
5. Kaffeina inaweza kuwa mlinzi kwa Ini
Ini ni ogani ya pekee sana mwilini na ina kazi nyingi mhimu sana kwa mwili.
Magonjwa kadhaa yanaathiri ini moja kwa moja kama vile hepatitis A, B na C, magonjwa ya mafuta katika ini na mengine kadhaa.
Mengi ya magonjwa haya hupelekea makovu kadhaa katika ini hali ijulikanayo kwa kitaalamu kama ‘cirrhosis’.
Watu wanaokunywa chain a kahawa wana asilimia mpaka 80 za kutokupata magonjwa mbalimbali ya ini.
6. Kaffeina inaweza kukuondolea msongo wa mawazo
Msongo wa mawazo au mfadhaiko ni ugonjwa hatari ambao unaweza kukupunguzia ubora wa maisha yako.
Ni hali ya kawaida kwa miaka ya sasa huku ikiathiri karibu asilimia 4 ya watu.
Katika utafiti mmoja uliofanywa na chuo kikuu cha Harvard Marekani mwaka 2011 iligundulika wanawake wanaokunywa kahawa na chai vikombe viwili mpaka vitatu kwa siku walikuwa na kiasi kidogo sana cha uwezekano wa kupatwa na mifadhaiko (stress).
Utafiti mwingine ukihusisha watu 208,424 ulionyesha watu wanaotumia chai na kahawa wana uwezekano wa mpaka asilimia 53 wa kutokujiingiza na matendo ya kujiua au kujinyonga wenyewe.

Maoni