Gigy Money: Young Dee Punguza Mitandao ya Wanawake Tulia na Amber Lulu Anakupenda Sana


Muuza nyago katika video mbalimbali za Bongo aliyejitosa katika muziki wa Bongo Flava, Gigy Money amemshauri Young Dee kupunguza mitandao ya wanawake.

Gigy Money ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake ‘Papa’ ameiambia E-Newz ya EATV kuwa kutokana na umri wake ni vema angetulia na aliyekuwa mpenzi wake, Amber Lulu.

“Kiukweli apunguze mitandao ya wanawake unajua ina mchanganya halafu ukiangalia umri wake mdogo angetulia tu na Amber Lulu kwa sababu anampenda sana,” amesema Gigy Money.

Ameongeza kuwa katika wanawake mia wanaompenda Young Dee Lulu ndio anampenda sana na wengine majina tu, huku akieleza kuwa wawili hao hawajahi kuachana kama inavyokuwa ikiripotiwa.

Maoni