MWANANCHI APIGWA RISASI WENZAKE WAANDAMANA:

Wananchi wa kijiji cha Mselesele kilichopo wilaya ya Ludewa mkoani njombe wameandamana hadi kwenye ofisi za kampuni ya YUSHING inayofanya kazi ya ujenzi wa barabara ya Njombe Ludewa kufuatia kupigwa risasi kwa Mfanyakazimwenzao
anaefahamika kwa jina la Haji Athuman kwa madai ya kuiba mafuta.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrea Tselle amesema kuwa amepokea taarifa hizo majira ya saa mbili asubuhi kuwa askari huyo wa ulinzi anaeitumikia kampuni ya Yushing inayojenga barabara ya kutoka Lusitu hadi Mawengi amefanya tukio hilo la kupigwa risasi kijana huyo kwa kushinikizwa na boss wake anaefahamika kwa jina moja la SAMYU.

Maoni