Nikki wa Pili ataja vipaumbele vyake 8 siku akiwa Rais | October 25, 2017

Msanii wa kundi la Weusi, Nikki wa Pili ameeleza vipaumbele vyake nane iwapo siku moja atakuwa Rais wa nchi.
1. Kikaoo kikubwa cha serikali yangu sio baraza la mawaziri itakuwa mkutano mkuu wa kijiji/ mtaaa (kitaa kinaongea)
2. Kipimo cha maendeleo kitakuwa kupanda au kushuka kwa maisha ya watu sio vipimo vya kukua kwa uchumi, makusanyo au shilingi.
3. Mfumo wa elimu utajikita kupima “learning” yani kujifunza sio kupima ufaulu na ufeli
4. Vyama vyenye nguvu vitakavyo kuwa vinafanya mikutano na kuihoji serikali sio vyama vya siasa bali vyama vya wakulima, wafanyakazi, walimu, machinga, boda boda, madaktari nakadhalika.
5. Serikali itakuwa mdau namba moja kwenye uchumi na mwekezaji atakuwa mkulima, mfugaji, mchimbaji mdogo, wavuvi wadogo na wafanyabiashara wa wadogo.
6. Ardhi, elimu, maji, afya havitakuwa bidhaa bali hifadhi ya jamii.
7. Maisha bila maadili hayana mana kila mtoto lazima afundishwe kuwa na adabu, uaminifu, heshima, ujamii, upendo, bidiii na kujiamini.
8. Mahusiano na mataifa ya Afrika, hakutakuwa na neno wahamiaji haramu, Mwafrika hawezi kuwa haramu Afrika ni nyumbani kwao.
Hata hivyo ameleeza kuwa maswali ataulizwa wakati wa kampeni ukifika lakini akiwa kama mgombea binafsi.

Maoni