SIMBA KAMBINI KUIWINDA MTIBWA SUGAR KATIKA MWENDELEZO WA LIGI KUU

Baada ya mapumziko kupisha mechi ya kimataifa kati ya Tanzania na Malawi, kikosi cha Simba kitarejea mazoezini leo kuanza kujiandaa na mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo utakaopigwa J/pili ya tarehe 15-2017 wiki hii.
Kikosi hicho kilikuwa katika mapumziko ya muda baada ya kucheza mechi dhidi ya Ligi dhidi ya Stand United mchezo ambao Simba ilishinda kwa jumla ya goli 2-1 goli zilizoipandisha mpaka kuwa namba moja kwenye msimamo wa Ligi.
Kikosi hicho kitaanza mazoezi kwenye Uwanja wa Polisi Kilwa jijini Dar es Salaam na imeelezwa mazoezi hayo yatafanyika kwa siku mbili mfululizo katika uwanja huo.
Vinara hao wa Ligi Kuu Bara wanaanza kujiandaa dhidi ya Mtibwa Sugar wanaoonekana kuwa na mwendo mzuri katika Ligi hiyo iliyo na ushindani mkubwa msimu huu.
Simba inaenda kuivaa Mtibwa Sugar ambayo mpaka sasa ina rekodi nzuri ya kutopoteza mchezo mmoja mpaka anacheza mchezo wa tano huku Simba ikiwa imeshinda mitatu kudroo miwili.

Maoni