UEFA Yaanzisha Ligi Mpya yaTimu za Taifa


Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limeanzisha ligi mpya ya timu za taifa ambayo itaitwa ‘UEFA Nations League’.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku moja tu baada ya kumalizika kwa michezo ya kuwania kufuzu kombe la dunia mwaka 2018. Ligi hiyo itaanza Septemba 2018 wakati ratiba itapangwa Januari 24 jijini Lausanne, Uswis.
Ligi hiyo mpya itakuwa na muundo wa ligi nne ambapo timu zitapangwa kutokana na uwezo wake. Ligi A itakuwa na timu 12 zinazoongoza kwa viwango vya FIFA ikifuatiwa na Ligi B ambayo nayo itakuwa na timu zinazofuata kwenye viwango baada timu 12 za mwazo huku Ligi C ikiwa hivyohivyo sambamba na Ligi D.
Katika Ligi A na Ligi B timu zitapangwa kwenye makundi matatu yenye timu nne kila kundi wakati Ligi C na B zitakuwa na makundi manne yenye timu nne kila kundi. Kwenye ligi hii timu zitakuwa zinashuka na kupanda kutoka ligi moja kwenda nyingine ikitegemeana na matokeo.

Ligi A: Germany, Portugal, Belgium, Spain, France, England, Switzerland, Italy, Poland, Iceland, Croatia, Netherlands.
Ligi B: Austria, Wales, Russia, Slovakia, Sweden, Ukraine, Republic of Ireland, Bosnia and Herzegovina, Northern Ireland, Denmark, Czech Republic, Turkey.
Ligi C: Hungary, Romania, Scotland, Slovenia, Greece, Serbia, Albania, Norway, Montenegro, Israel, Bulgaria, Finland, Cyprus, Estonia, Lithuania.
Ligi D: Azerbaijan, FYR Macedonia, Belarus, Georgia, Armenia, Latvia, Faroe Islands, Luxembourg, Kazakhstan, Moldova, Liechtenstein, Malta, Andorra, Kosovo, San Marino, Gibraltar.

Maoni