Unaweza kusema kusharekea siku ya kuzaliwa Bongo, yahitaji moyo

Unaweza kusema kusharekea siku ya kuzaliwa Bongo, yahitaji moyo.

Tokea wazungu walivyoanza kumwagiana maji wakati wa sikukuu ya kuzaliwa maarufu kama Birthday, Bongo nao wamebuni yao, wao wanamwagiana matope.

Mchezaji Godfrey Taita ambaye ni beki mkongwe wa Kagera Sugar anaweza kuwa mfano wa hilo tena ni siku chache kabla ya kuivaa Yanga.

Kagera itashuka dimbani wikiendi hii kwenye Uwanja wa nyumbani kwao wa Kaitaba kuwavaa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga.

Wakati Kagera Sugar inajiandaa kuivaa Yanga wikiendi hii, Taifa jana alikumbana na mkasa wa kumwagiwa matope na wachezaji wenzake.


Tukio hilo liliongozwa na beki Mohamed Fakhi na Japhet Makaray ‘Balotelli’ kuhakikisha Taifa anaoga matope ya kutosha.

Taifa ambaye aliwahi kuichezea Yanga alionyesha kuwa mpole wakati wa zoezi hilo lililomfanya kuonekana kama “kinyago cha mpingo”. 

Maoni