WAKATI wanaume wao wakivuja jasho uwanjani, wake wa wachezaji mpira Ligi Kuu, wamejiongeza na kuanzisha umoja wao kwa ajili ya kusaidiana shida na raha ili mambo yao yawanyookee.

WAKATI wanaume wao wakivuja jasho uwanjani, wake wa wachezaji mpira Ligi Kuu, wamejiongeza na kuanzisha umoja wao kwa ajili ya kusaidiana shida na raha ili mambo yao yawanyookee.
Umoja huo ambao una zaidi ya wanachama 15 ukiongozwa na mke wa kipa Shaaban Kado, aitwaye Brandy pamoja na yule wa beki Geofrey Taita, Asha Mabruk.
“Lengo la kuunda umoja huu kwa ajili ya kusaidiana shida na raha pamoja na kupeana maana katika maisha kuna mambo mengi.
ADVERTISEMENT
Tumejiwekea malengo na moja wapo ni kuchangia mfuko kila mwezi kiasi cha Sh20,000 kwa kila mmoja wetu,” alisema Brandy aliyefafanua umoja wao ndio umeanzishwa sasa na watakuwa wakikutana kila mwezi.
Miongoni mwa wajumbe hao ni pamoja na Ray wa Tambwe, Mke wa Amissi Tambwe, Nance wa Kelvin Yondani, Leyla Kapemba wa Pius Kisambale, Gracia Nebbo wa Juma Seif ‘Kijiko’, Zamda Bakary wa Said Mohamed ‘Nduda’, Happiness Edward wa beki wa Simba, Ally Shomary. Wengine ni Pendo Kavila wa George Kavila, Mariam Said wa Jackson Chove, Aisha Luhende wa David Luhende, Hyma Honey wa Abdallah Seseme.

Maoni