Watano wafariki katika majibizano ya risasi

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Emmanuel Lukula ameeleza kwamba  walipata taarifa ya kutokea kwa tukio hilo kutoka kwa wasamaria wema kuwa kuna mikakati ya uhalifu imepangwa kufanyika maeneo hayo usiku wa jana, hivyo wakajipanga kwa ajili ya kudhibiti.
Amesema kwamba baada ya muda walioambiwa ulipofika wahalifu hao wengi ambao idadi yao haikupatikana walifika eneo la tukio na kukutana na polisi kisha kuanza kupambana.
“Majibizano ya silaha yalikuwa makubwa kwa sababu walikuwa na silaha nzito, lakini Jeshi la Polisi lilijipanga imara kuwadhibiti na kufanikiwa kuwauwa watano na wengine wakatokomea kusikojulikana,” amesema.
Aidha Kamanda wa polisi ameongeza kwamba “Tumejipanga na tunapopata taarifa za uhalifu, pamoja na askari wetu kuwa doria maeneo hayo, lakini hujipanga upya kwa ajili ya kupambana na tukio husika. Wananchi wasiwe na hofu kutoa taarifa kwani jeshi la polisi lipo tayari kulinda raia na Mali zao.

Maoni