YANGA NA SISI TUNAWALETA WANAWAKE

Klabu ya Yanga ambayo kiasili ni Taasisi ambayo inajihusisha na Michezo na siyo soka Peke yake ndiyo maana inaitwa Yanga Sports Club (SC) na Siyo Yanga Football Club (FC) wakimaanisha wanajihusisha na michezo yote licha ya kuwa wamesimama zaidi kwenye soka hususani la Kiume kwa miaka mingi.
Leo klabu ya Yanga msomaji wa Shabanirapwiblogsport.com waliitisha mkutano na waandishi wa Habari na moja kati ya mambo ambayo walipata nafasi ya Kuyaongelea ni mpango wa Kuja na timu ya wanawake ya Yanga.
Kupitia kwa mmoja kati ya wajumbe wa kamati ya Utendaji Siza Lyimo amesema kuanzia leo wanakaribisha wanawake wenye mapenzi mema na Yanga na wenye uwezo mzuri na Mkubwa wa kusakata kabumbu kwaajili ya kufanya majaribio mpaka tarehe 30 mwezi huu Oktoba na baada ya hapo utaratibu mwingine Utafata.
Yanga wanakuja na mpango huu siku kadhaa baada ya watani wao timu yao ya wanawake kufanikiwa kupanda ligi kuu ya wanawake Nchini.

Maoni