AFISA MTENDAJI KATA GOBA " JUKUMU LA ULINZI NA USALAMA WA GOBA NI LA WANAGOBA WENYEWE ".

Afisa Mtendaji wa Kata ya Goba Ndg. Hamatton Bhao ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kundi la vijana wazawa wa Kata hiyo ambao aliwaandalia mafunzo ya Ulinzi Shirikishi katika kata ya Goba.
Uzinduzi huo umefanyika leo Jumatano 29/11/2017 katika uwanja wa mpira wa miguu wa shule ya Sekondari Goba na kuhudhuriwa na Afisa wa Polisi jamii Mkoa wa Kipolisi Kinondoni A.G Sempombe , ASP akiambatana na mkuu wa kituo cha Polisi Kawe ASP Mwambungu pamoja na Inspekta John Ntunde ambaye ni Polisi Jamii Tarafa ya Kawe pia Wenyeviti wa mtaa wa Goba na Muungano.
Kundi hilo ambalo limeundwa kutokana na mitaa mitatu Iina jumla ya vijana 42 wakiwemo wanaume 41 na mwanamke mmoja wote wakiwa na umri kuanzia miaka 18 hadi 45.
Kata ya Goba ni moja kati ya Kata 14 zinazounda Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ambayo inaongozwa na Mkurugenzi Ndg. John Lipesi Kayombo.
Katika kuhakikisha tunamsaidia Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Kata ya Goba imekuwa mfano kwa Kata zingine katika suala la ulinzi shirikishi ili kuyawezesha maeneo yake yanakuwa shwari.
Bhao amebainisha mafunzo hayo ya Ulinzi Shirikishi kwa kata ya Goba lazima yafanyike katika mitaa yote nane inayounda Kata ya Goba kwa sasa tumeanza na Mitaa mitatu (3) ambayo vijana wake wanapatiwa mafunzo mitaa hiyo ni Goba, Muungano na Matosa.
Kwa upande wa suala la ulinzi na Usalama ni lazima tuhakikishe vijana wetu wanapatiwa mafunzo katika mitaa yote nane na jambo hili ndugu zangu ni la kizalendo mi Mtendaji wenu wa kata ambaye namuwakilisha Mkurugenzi nitakuwa bega kwa bega nanyi alisema Hamatton bhao.
Amesistiza natamani kuona kila kijana katika Kata yangu anashiriki kwa namna moja au nyingine katika shughuIi za kizalendo za kujenga nchi.
Mwisho Bhao amemshukuru Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo ndg John Lipesi Kayombo kwa Ushirikiano wake katika kazi na kuahidi atatumia uwezo wake na karama aliyopewa na mwenyenzi Mungu kuhakikisha hamuangushi Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo na Goba inasonga mbele.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.

Maoni