Alikiba na Nandy washinda tuzo AFRIMA 2017

Usiku wa kuamkia leo nchini Nigeria kulitolewa tuzo za All Africa Music Awards 2017 (AFRIMA) ambapo wasanii wawili kutoka Bongo, Alikiba na Nandy wameibuka washindi.
Alikiba ameshinda Tuzo mbili katika vipengele vya Best Africa Collaboration kupitia ngoma ‘Aje’ pamoja na kipengele cha Best Artist or Group in Africa RnB and Soul ambapo pia ni kupitia ngoma ya ‘Aje’ kwa kushirikiana na M.I.
Wakati huo Nandy akishinda katika kipengele cha Best Female Artist In Eastern Africa Award. Wasanii wengine wa Tanzania waliokuwa wakiwania ni pamoja na Feza Kessy na Vanessa Mdee.

Maoni