AZAM YATUMA SALAMU

TIMU ya Azam FC, usiku wa Jumatano imeichapa Ashanti United mabao 4-0, katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Azam Complex.
Mchezo huo ulikuwa ni mahususi kwa ajili ya kuwaweka kwenye ushindani wachezaji, pia wakipasha misuli kuelekea mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Ruvu Shooting utakaofanyika uwanja huo Jumamosi hii saa 1.00 usiku.
Azam FC ilifanikiwa kutawala vipindi vyote vya mchezo huo, huku benchi la ufundi likichezesha vikosi viwili tofauti katika kila kipindi cha mchezo huo, isipokuwa wachezaji wawili beki wa kulia, Swaleh Abdallah na kiungo Masoud Abdallah, ambao ni majeruhi.

Maoni