DIWANI WA KATA YA CHAMAZI ATOA JEZI KWA VIJANA WA....

Diwani wa kata ya chamazi Mh Hemedi Karata leo tarehe 26/10/2017 amekabidhi jezi kwa makundi manne ya ukimbiaji (jogngg)   ambayo ni Vijana Combine Jog, Rufu Jog, Mbande Jog na Kisewe Jog .

Huu ni utaratibu ambao  Mh. Diwani na UVCCM kata ya chamazi ambao wamejiwekea wa kukusanya vijana kila jumapili ya mwisho wa mwezi hivyo Basi wameitumia siku ya Leo kwa ajili ya ugawaji wa jezi hiyo pamoja na kuzinduliwa kwa jogging ya tawi la Dovya A.

Akizungumza kwa niaba ya vijana hao katibu wa UVCCM kata ya chamazi Ndg Juma Bega Zonzo amemshukuru diwani kwa kitendo chake cha kukaa karibu na vijana kwani ndio kasi inayotakiwa katika awamu hii ya tano nae Yupo tayari kushirikiana na diwani kwani ndo lengo kubwa la kila mwanaccm kuhakikisha ilani ya chama cha Mapinduzi inatekelezwa ipasavyo.

Maoni