Faida 20 za mazoezi ya kutembea

1. Mazoezi husaidia kupunguza uzito, tembea saa mmoja kila siku
2. Ni mazoezi yanayoweza kufanywa na kila mtu
3. Ni mazoezi yasiyohitaji vifaa/ hayana gharama
4. Ndiyo njia rahisi kabisa kuufanya mwili kuwa mkakamavu
5. Hupunguza dalili za majonzi na wasiwasi
6. Ni mazoezi yenye matikeo ya taratibu
7. Hupunguza uwezekano wa kupatwa na kolesto/ lehemu
8. Hupunguza na kutibu shinikizo la damu
9. Hupunguza uwezekano wa kupatwa na baadhi ya kansa
10. Hupunguza uwezekano wa kupatwa na kisukari
11. Hukufanya ujisikie vizuri
12. Husaidia kuimarisha mifupa
13. Husaidia kupunguza uwezekano wa kupatwa na shambulio la moyo
14. Ni mazoezi uwezayo kuyafanya bila kukusababisha ajari au maumivu makubwa
15. Hupunguza mafadhaiko/ stress
16. Hupunguza uwezekano wa kapatwa na ugonjwa wa moyo
17. Ni mazoezi unayoweza kuyafanya bure bila kuulipia chochote
18. Husaidia katika mfumo wa upumuwaji
19. Husaidia kuongeza mzunguko wa damu
20. Husaidia kuimarisha mishipa
Kama afya yako siyo nzuri sana anza kutembea kidogo kidogo labda dakika 10 kwa siku huku ukiongeza dakika 5 kila siku hadi hapo utakapoweza kutembea saa mmoja mfululizo bila kupumzika. Ili kupunguza uzito, unene, utipwatipwa, mafuta yaliyozidi au kitambi, fanya zoezi la kutembea kwa miguu mwendo kasi kidogo muda wa mwezi mmoja mpaka miwili mfululizo.
Je, ni muda gani mzuri wa kufanya mazoezi ya kutembea?
Wengi wanapenda asubuhi sana na jioni lakini mimi napenda kufanya mazoezi ya kutembea mchana wakati wa jua kali saa sita, saa saba au saa nane, tena huwa natoa kabisa shati na kubaki tumbo wazi. Utanishangaa kwa nini na fanya hivi, jua lina muhimu sana kwa afya ya mwili na ngozi pia kama chanzo cha vitamini D, vitamini ambayo ni muhimu sana katika kuimarisha mifupa na hivyo kuzuia ugonjwa wa mifupa (osteoporosis), kuzuia maumivuya mishipa, kushusha shinikizo la damu, kudhibiti kisukari, kudhibiti kolesto na kudharka. Unapotembea mchana wa jua kali unaruhusu jua kutua juu yako mwili mzima.

Maoni