Hawa ndio watakaosafiri na Taifa Stars, kuifuata Benin.

International Friendly:

Timu ya soka ya Taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’ inatarajia kuondoka nchini, Alhamisi hii ya Novemba 9 kwenda nchini Benin kwa ajili ya mchezo wao wa kimataifa wa kirafiki uliopo kwenye kalenda ya FIFA.

Afisa Habari wa Shirikisho la soka nchini TFF, Alfred Lucas Mapunda amesema wachezaji wote waliopo kambini wapo katika hali nzuri na kwamba kikosi hicho kitasafiri bila ya kuwepo kwa Mbwana Samatta pamoja na Abdi Banda.

-Kikosi cha timu yetu ya Taifa kinatarajia kuondoka hapa Alhamisi alfajiri kwenda Benin kwa ajili ya mechi yao ya kimataifa ya kirafiki na kitakapofika rasmi kesho yake kitaendelea na programu yake mazoezi huko Benin,” alisema Lucas.

Watakaosafiri.

Wachezaji watakaosafiri ni Aishi Manula, Peter Manyika, Gadiel Michael, Boniphas Maganga, Kelvin Yondani, Nurdin Chona na Himid Mao.

Wengine ni Hamis Abdallah, Raphael Daudi, Mohamed Issa ‘Mo Banka’, Jonas Mkude, Mudathir Yahya, Simon Msuva, Shiza Ramadhan Kichuya, Faridi Mussa,  Ibrahim Ajib, Mbaraka Yusuph na Elias Maguli.

Mchezo huo wa kirafiki utafanyika Novemba 12 katika uwanja wa Stade de l'Amitié uliopo katika mji wa Cotonou.

Maoni