JUMA AYO andika uwaraka kwa TFF juu ya uwamuzi wa Wilfred Kidau

Juma Ayo ni mtangazaji wa kipindi cha michezo kwenye radio ya jembe fm 93.7 mwanza ameandika uwaraka uwo kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook nukuu-
"WARAKA KWA TFF
Anaandika JUMA AYO!
Leo kaimu Katibu Mkuu wa Tff Wilfred Kidau amezungumza na wanahabar juu ya masuala mbalimbali likiwemo suala linalosambaa mtandaoni juu ya viongz wa taasisi hiyo kubwa nchini kukunja mamilion ya pesa
Nimpongeze kaimu Katibu Mkuu kwa kutoa ufafanuzi mzuri kabisa ,pengine ni Mara ya kwanza kwa TFF mpya kuanzia kujibu hoja mbalimbali dhidi yao na kama wataendelea hivo hakika mtafanikiwa kwa kiasi kikubwa kuliko kukaa kimya kuendelea kutengeneza hoja kwa familia ya mpira..
Bado nimeendelea kuwaza kwani TFF ya zamani ya Tenga,Mpaka Jamal malinzi viongz walikuwa wanalipwaje? Posho ,mishahara nk?
Kwanini hakukuwahi kutokea migogoro ya kujadili Rais achukue kiasi gani? Au Katibu achukue kiasi gani?
Hii inatoa tafsir kwamba pengine safar hii kulikwepo na mfumo mpya wa ulipwaji wa watendaji ndani ya taasis hiyo ndo maana muafaka haukupatikan juu ya kiasi gani rais achukue !!!
Na kama rais hakuwa tayar kuchukua pesa hizo nani alieleta hoja viongz hao wa juu walipwe pesa hizo?(bado naendelea kutafakar)
Kaimu umeelezea mambo mazuri sana japo mwisho nimepingana na wewe juu ya kuwachukulia hatua baadhi ya waandishi walioandika hama kusambaza taarifa hizo ....
Siku zote hoja hupingwa kwa hoja,tafiti hupingwa kwa utafiti na hicho ndicho mlichokifanya Leo kuja mbele ya watz na kutuweka wazi kama mojawapo ya ilani ya rais aliyeko madarakan ndg Wallace Karia (uwazi)
He mnafikir mkiwachukulia hatua watu hao ndo suluhisho katika kukuza mpira wetu?...je watz wangejua kama masuala haya mliyajadili bila waandish hao kuchimbua yanayoendelea hata kama hakukuwa na ukweli?
Mpira wetu hauwezi kusonga bila ya waandish wa habar kuandika positive or negative ya yanayoendelea
Tunaomba mlitafakari sana kiundani hili ....nawaza tu endapo waandish hawa watachukuliwa hatua je waandish wengine watakuwa na mapokeo gani kwenu ?
Na je mnafikir wataendelea kufurahia kuja karume kuhudhuria mikutano yenu wakati wenzao wamo ndani? Au wana misukosuko?
Tanzania kila MTU ni tatizo kubwa tuvumiliane katika matatizo yanayotukabili na tutiane moyo
Tff hamwezi kufanikiwa bila kupitia haya ,mtasemwa,mtaandikwa,mtasingiziwa,mtasifiwa pasipostahili sifa lkn lazima maisha yaendelee
Waandish wana mambo mengi sana juu ya mpira wa nchi hii najua wakiamua kupaza sauti pengine kila MTU ataonekana ni tatizo" kisha akamalizia kwa kuandika
"Naomba kuchukua fursa hii kuwatia waandishi moyo kuendelea kufanya kazi bila kuchoka lakn tuendelee kuzingatia miiko ya uandishi !!!!!
NO ONE IS PERFECT"

Maoni