CHAMAZI KUTII AGIZO LA MH RAIS MAGUFULI

Leo Jumamosi 25/11/2017 katika kata ya CHAMAZI kulikuwa na zoezi la usafi katika eneo la DOVYA A.

Takribani vikundi 6 vya vijana (jogging) vilijumuika pamoja kufanya usafi katika maeneo ayo.

Yote hayo ni katika kutii agizo la kufanya usafi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi.

Agizo lilotelewa na Rais Dk John Pombe Magufuli 

Zoezi ilo la usafi liliongozwa na viongozi kadha wa Chama Cha Mapinduzi akiwepo Ndg.  JUMA BEGA  pamoja na viongozi wengne wa CCM wa mtaa huo wa Dovya A. pamoja na Katibu Hamasa na Chipuki Kata ya Chamazi Ndg NAJIM NURDIN NYANZA akiwa na Rais wa vijana wa kata ya chamazi Ndg NASRI MKAPIRA na wadau wa Chama Cha Mapinduzi.

Baada ya kukamilika zoezi la usafi  Mdau wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Mjungu alipata frusa ya kuzungumza na vijana hao na kutoa ahadi ya kuwasaidia vifaa vya michezo ikiwepo jezi na n.k

Pia licha ya kutoa ahadi iyo Ndg Mjungu alisema kuwa yupo tayali kuwasaidia vijana wasio na ajira.
Nukuu "Jun nitaitaji vijana sita walio fika mpaka fom 4 na wanaleseni,pia nitaitaji mabint 20 kwa mabint sitaangalia kingezo kikubwa sana kama umefika fom 4 inatosha naitaji niwategeneze frusa, msiwe mnakimbia na kufanya mazoezi pasipo kuwa na malengo au mising sasa nawatangazia iyo frusa,na frusa hii inapatikana ukiwa kwenye vikundi kama ivi maana siwezi kumfata mtu mmoja mmoja,alisema Ndg Mjungu.

Pia baadh ya vijana nao walitoa maoni yao akiwepo Rajabu Salehe  Nukuu" Sisi kama vijana wa kata ya chamazi tunamuunga mkono Rais wetu Magufuli kwa  utendaji kazi wake ndio maana leo hii tumetii agizo lake la kila jumamosi ya mwisho wa mwezi usafi" alisema kijana uyo.

Maoni