Mh Lazaro Nyalandu afunguka mazito juu ya yeye kutoka CCM

Nukuu "Wakati naondoka CCM, nililijulisha TAIFA kuwa naamini kwamba, Tanzania inahitaji kupata Katiba Mpya, na kwamba tufanye rejea ya RASIMU ya mapendekezo ya Katiba ya Tume ya Warioba ili pamoja na Mambo mengine, kuwepo mgawanyo kamili wa madaraka katika mihilimi ya utawala wa Chini (Bunge, Serikali, na Mahakama), na kuondoa muingiliano na kuweka ukomo wa madaraka wa wazi kwa kila muhimili, ili mwisho wa yote, wenye madaraka kamili ya nchi wabaki kuwa wananchi wenyewe;

Ndugu wana Mwanza,
Nikiwa hapa kuwaomba kura za NDIYO kwa Mgombea UDIWANI wa Chadema kwa Kata hii pendwa, 
Naomba kulikumbusha Taifa kuwa katika umoja wetu, tutaishinda hofu, tutaushinda utengano na tutaimarisha demokrasia ya kweli hapa nchini Tanzania.

Na Sasa Saa imefika, na Saa hiyo ndio Sasa, Watanzania tusinung’unike tena, tusiwe na simanzi tena, na tusihuzunike tena, kwa kuwa MUNGU ameruhusu miongoni mwetu, na kwa wote mnaoyasikia MANENO haya, kuamsha mashujaa watakao simama na kuitetea haki Tanzania.

Hakika, Saa imefika ambapo, yeyote ajionaye mnyonge na dhaifu miongoni mwetu na asimama, AKIRI akisema MIMI ni shujaa, kwa kuwa Saa ya mabadiliko inakuja!

Naam, Saa imefika kwa mtu yeyote miongoni mwetu aliye maskini na akiri, MIMI ni tajiri, kwa kuwa ndani yetu, na katika ukiri wetu, tumepewa utayari wa kuiambia Tanzania, MUNGU wako anamiliki. Tumepewa uwezo katika ukiri wetu, wa kubadilisha mwelekeo wa nchi, na kuiambia Tanzania kwamba, wewe nchi ni iliyo chini ya MUNGU Moja, lakini ameruhusu UTAJIRI na Wingi wa mawazo mbadala. Kila Moja wetu, asiogope!

MUNGU Ameruhusu Sasa, Chadema isimame, ikiwa pamoja na vyama vingine vya Upinzania, kama Chama Cha Watanzania wote, bila kujali dini zao, bila kujali makabila yao, na bila kujali mapokeo ya itikadi zao za Kisiasa, ili kuleta mabadiliko mapya ya kiuchumi, kijamii, na kisiasa.

Kwa kuwa imeandikwa katika vitabu zamani, ni “Mizuri kama nini, miguu yao waletayo Habari njema.” Kwa Mwanza, na Tanzania, na kwa wote waliosimama Katika Mkutano huu Mkubwa, tunawatangazia Uhuru kwa wale wasiojisikia huru kuongea, tumekuja kuwatangazia wote walio wapole wa kunena, wasije kunyamaza tena, kwa kuwa SOTE tunaungana kukiri kwa mara nyingine tena, Tanzania"

Maoni