Mh Nyalandu Ampongeza Uhuru Kenyatta

Baada ya kuapishwa Uhuru Kenyatta watu mbalimbali wakiwepo wanasiasa, Viongozi wa Dini, Wasanii na watu Maarufu wakimpongeza na wakimtakia baraka na uwongozi mwema na moja kati ya hao akiwepo Mh Nyalandu aliandika kupitia ukurasa wake wa facebook akimtakia baraka na uwongozi mwema Kenyatta na Makamu wake Wiliam Ruto
Nukuu "
NIMEWASILI Ikulu ya Nairobi, Kenya kuhudhuria hafla ya chakula cha mchana kufuatia kuapishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta na Makamu wake William Ruto katika uwanja wa Kasarani kuongoza Jamhuri ya Kenya katika kipindi cha pili. Namtakia Rais Uhuru na Mama Margaret, pamoja na Makamu wake Ruto na Mama Rachel afya njema na Baraka za MUNGU katika kuwaongoza Watu wa Kenya kwa amani, haki, na maendeleo kwa wote. # InauguarationKe"

Maoni