MWAKYEMBE AWAAMBIA KILI STARS WAMTANDIKE YOYOTE MBELE YAO CHALENJI



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harison Mwakyembe, isiku huu akipata fursa ya Kula chakula cha pamoja na wachezaji wa kikosi cha Taifa Taifa Stars ndani ya Sisicape Hotel iliyopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

Mwakyembe alitumia muda huo kuwaaga wachezaji hao ambapo kesho  asubuhi wanaenda nchini Kenya kushiriki katika michuano ya Kagame Cup.



Akiwaaga kwa pamoja amewataka wayatumie mashindano hayo kuiletea Tanzania heshima ya ubingwa kwani wana kila sababu ya kufanya hivyo kwani Serikali ipo pamoja nao huku akiwata wahakikishe wanashinda kila mchezo uliyo mbele yao.

"Ninatambua uwezo wenu ni mkubwa kama Mwalimu alivyosema hakikisheni mnamtandika kila atakae kuja mbele yenu mimi nitakuja mchezo wa pili mkishinda.

"Makipa watatu nawajua wako poa lakini hata Straika wako safi na beki nawajua wachache lakini wapo safi

Hivyo hadi hapo sina wasiwasi na mchezaji yoyote kati yenu zaidi mcheze mkitajua Watanzania wapo nyuma yenu na wanahitaji ushindi wa ngumu," alisema Mwakyembe


Kikosi hicho leo kimeongeza wachezaji watatu wapya ambao ni Yahaya Zaydi (Azam)nafasi ya Straika,

Amani Kaita (Nakuru All Stars Kenye) anacheza nafasi ya kiungo na  Ramadhani Kabwili kipa wa Yanga.

Maoni