NASRI MKARIPA MWENYEKITI UVCCM KATA YA CHAMAZI ATOA PONGEZI KWA MADIWANI WATEULE

Mwenyekiti Uvccm kata ya chamazi  Ndg Nasri Mkapira ametoa pongezi za dhati kwa madiwani wote wateule, pongezi  izo amezitoa kupitia ukurasa wake wa Facebook kwa kuandika yafuatayo
Nukuu:_
"PONGEZI ZANGU ZA DHATI KWA WAHESHIMIWA MADIWANI WATEULE.

Asalaam aleykum...

Bwana Yesu asifiwe.........

Natumai ni wazima wa afya.

*Jana Jumapili 27 November 2017 kulifanyika uchaguzi mdogo wa marudio katika ngazi ya UDIWANI*.

Uchaguzi huo ulikuwa ni katika kujaza nafasi za Udiwani zilizokuwa wazi kutokana na sababu mbalimbali kama kifo, pingamizi n.k.

Uchaguzi huo Kata ulihusisha Kata 43 zilizokuwa hazina MADIWANI nchi nzima.

Uchaguzi uligubikwa na matukio mengi sambamba na maneno ya hapa na pale kama ilivyo kawaida bila vitu hivyo uchaguzi haunogi ni sawa na mpira wa miguu bila kelele za mashabiki.

Kama ilivyo ada nchi yetu imejikita katika misingi ya amani na utulivu ambayo iliasisiwa na Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Uchaguzi ulifanyika na umekwisha  kwa amani japo kuna misuguano ya hapa na pale hivyo havikosi kwani hata vikombe kabatini vinagongana.

Baada ya kufanyika uchaguzi wananchi wakawachagua wawakilishi wao (MADIWANI) ambao watadumu kwa kipindi cha miaka mitatu *2017-2020*.

Hongereni nyote mliopata ridhaa ya wananchi ya kuwatumikia.

Mkafanye kazi kweli na kutimiza yote mliyowaaidi kwani siasa za zamani za *UONGO* mwingi zimepitwa na wakati.

Fuatisheni anachokifanya Rais wetu mpendwa Mh. John Pombe Magufuli.

Kwani yeye ana huruma na wananchi hususani wanyonge.

Nafasi hiyo waliitaka wengi ila nyinyi ndio Wananchi wamewataka naomba muwasikilize, muwajali na mtatue kero zao kwa wakati.

Wananchi wanawaangalia kwa macho matatu mkiyumba TU watawasubiri 2020 na wao wawayumbishe.

*MWISHO*

Hongereni sana Waheshimiwa MADIWANI wateule kwani kugombea ni jambo rahisi ila kushinda ni jambo kubwa na gumu.

Mkapeperushe vyema bendera ya Chama kilichokuteua na hatimaye kuchaguliwa na wananchi.

Pia mkumbuke *MAENDELEO HAYANA CHAMA* mkawatendee haki wananchi wote hata wale wasio wa Chama Chako.

Sina mengi " alisema Ndg. Nasri Mkapira

Maoni