Nini Hukumu ya Kuangalia Picha za Uchi, na za Ngono?

Swali: Rafiki yangu mmoja, kila aingiapo ‘Cafe”, kazi yake ni kusachi tovuti za ngono. Nini hukumu ya jambo hilo, na nifanye nini kumuepusha na tabia hiyo mbaya?

Jawabu: Hairuhusiwi kutazama picha za uchi zinazoonesha sehemu za mvuto na za utupu wa wanawake, ama iwe katika tovuti za mitandao, magazeti, majarida na kadhalika. Hii ni kwa sababu, kuzitazama picha hizo ni njia mojawapo ya kuwafaidi wanawake hao na kuujua uzuri walionao.

Hii pia yaweza kuwa njia ya kumpelekea mtu kutenda mambo ya haramu, hivyo, inahukumiwa kuwa ni njia haramu, kwa sababu chanzo cha jambo kinahusishwa na hukumu ileile inayohusu hatima ya jambo hilo.
Â
Watu wengi hulichukulia kirahi-rahisi jambo hili la kuangalia picha za uchi za wanawake wasiokuwa maharimu zao, kwa hoja kuwa hizi ni picha tu na si vitu halisi. Lakini hili ni jambo baya sana kwani linamshawishi (linamuhamasisha) mtu kuthubutu kumchungulia mwanamke ili amuone moja kwa moja alivyo.
Â
Mwenyezi Mungu anasema, “Waambie Waislamu wanaume wainamishe macho yao (wasitazame yaliyokatazwa), na wazilinde tupu zao, hili ni takaso kwao; bila shaka, Mwenyezi Mungu Anazo habari za (yote) wanayoyafanya.� (24:30).
Â
Unaweza kumsaidia rafiki yako aepuke mambo hayo kwa kumnasihi mara kwa mara na kumuwaidhi amche Mungu, mkumbushe kuwa Mwenyezi Mungu muda wote humuona, na kwamba hakuna kinachofichikana Kwake.
Â
Na mkumbushe neema alizopewa na Mwenyezi Mungu kama vile macho ya kuonea vitu vya kumnufaisha, na Amemkataza kutumia macho hayo kuangalia mambo ya haramu.
Â
Muwaidhi kuwa Mwenyezi Mungu atakuja kumuuliza juu ya jambo hilo, ndio maana ya Mwenyezi Mungu katika aya iliyonukuliwa hapo juu anasema, “Yeye Anazo habari za yote wanayoyafanya (watu).�
Â
Aidha Mwenyezi Mungu anasema, “Hakika masikio na macho na moyo, hivyo vyote vitaulizwa.� (17:36).
Â
Mtu mwenye akili na busara akilitafakari jambo hili, pale anapoziangalia picha hizo za haramu, atatanabahi kuwa hakuna lolote la maana (analonufaika nalo) ila kujitia hasara, kujitesa bure na kusononeka tu kwani hawezi kuambulia chochote zaidi ya kukodolea macho tu picha hizo.
Â
Kajisemea kweli mshairi pale aliposema, “unapoyapa uhuru macho yako, hii itakupa bure mateso makubwa ya moyo.�
Â
Utaishia kuona tu kile ambacho huwezi kukipata, na utaishia kuhamanika (kuchanganyikiwa) kwani huambui kitu kwa kile unachokiona. Kwa hiyo, ni dhahiri kuwa hakuna kinachopatikana katika picha hizo ila ghadhabu tu za Mwenyezi Mungu, na mtu kupoteza muda na pesa bure kwa mambo yasiyompendeza Mwenyezi Mungu, na yanayomtesa yeye mwenyewe (kisaikolojia).
Â
Muislamu hana budi kuutafuta utwaharifu kwa njia ya ndoa, na ajikidhi kwa tamkini yake. Pia aepuke marafiki wabaya wenye ushawishi mbaya kwake ambao ndio wanaomshawishi kwenda cafe kwa ajili ya kutazama mambo hayo.
Â
Vilevile ajishughulishe na mambo yatakayomnufaisha kwa maana zote, duniani na Akhera, kama vile kuhifadhi Qur’an, kushiriki katika mambo ya kheri, kujipinda katika mambo ya kumkurubisha kwa Allah, na kufungua tovuti za maana zenye mambo ya kumuelimisha (na kumuadilisha).
Â
                Â             Allah Ndiye Mjuzi wa Yote
Â
Imejibiwa na Sheikh Muhammad S. al-Munajjid- Imamu wa Masjid Umar Ibn Abdul-Aziz. Alkhuber, Saudi Arabia.

Maoni