Rooney apiga hattrick yake ya kwanza Everton huku City wakiendelea kupeta

Wakiwa wametoka kumtangaza kocha mpya hii leo Everton wameibuka kidede kwa ushindi wa mabao 4 kwa 0 zidi ya klabu ya West Ham United wakiwa katika uwanja wao wa Goodison Park.


Wayne Rooney alikuwa shujaa baada ya kufunga hattrick ya kwanza akiwa na Everton huku ikiwa hattrick yake ya 9 katika maisha yake ya soka,bao lingine la Everton lilifungwa na Ashley Williams.


Arsenal wakiwa nyumbani waliichapa Huddersfield mabao 5 kwa nunge huku Olivier Giroud akifunga mabao 2 yanayomfanya kufikisha idadi ga mabao 151 katika maisha yake ya soka ngazi ya vilabu, 79 alifunga Ufaransa na 72 Uingereza.


Mo Salah ameendelea kung’ang’ania usukani wa vinara wa ufungaji baada ya hii leo kufunga mabao mawili wakati wakiiua Stoke City bao 3 kwa nunge huku bao lingine likifungwa na Sadio Mane.


Goli la dakika za mwisho la Raheem Sterling liliipa Manchester City alama 3 muhimu na kuzidi kuwaweka kileleni mwa ligi baada ya ushindi wa bao 2 kwa 1 na Southampton huku Chelsea kupitia Antonio Rudiger wakiichapa Swansea bao 1 kwa nunge. 

Maoni