Serikali yasaka mji wa kuandaa AFCON U17

Kwa ufupi
Tanzania kwa mara ya kwanza watakuwa wenyeji wa fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana U17 zitakazofanyika 2019
Habari THURSDAY, NOVEMBER 16, 2017
Serikali yasaka mji wa kuandaa AFCON U17

By Habel Chidawali

Dodoma. Serikali imesema bado haijachagua mji wa pili baada ya Dar es Salaam utakaotumika kwa ajili ya mashindano ya Afcon 2019 kwa Vijana chini ya miaka 17 (U17)
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza wakati anajibu swali la mbunge Elibariki Kingu (Singida Magharibi-CCM).
Katika swali lake mbunge huyo amehoji iwapo serikali imeteua mjini wa pili mbali na Dar es Salaam kwa ajili ya mashindano ya AFCON ya Vijana yatakayofanyika Tanzania.
Naibu Waziri Shonza alisema uteuzi maeneo yatakayotumika kuendesha mashindano hayo utafanywa na kamati ya maandalizi.
Alisema kamati iliyoundwa na kutangazwa na Waziri mhusika Novemba 11 inaendelea kuangalia uwezekano wa kuteua miji mingine ambayo itabeba jukumu hilo.
Kuhusu vigezo alisema lazima mkoa uwe na viwanja bora na mahoteli ya kuwezesha huduma kwa wageni.

http://www.mwananchi.co.tz

Maoni