Sister P Kurudi Kwenye Game

Sister P Kurudi Mzigoni, Atamani Kufanya Kazi Na Alikiba Mwanadada mkongwe katika game la muziki wa kizazi kipya sister p, ambae alikuwa kimya kwa kipindi cha muda mrefu ametangaza kuja na ujio mpya huku akitamani sana kufanya kazi na moja ya wasnii wanaofanya vizuri sasa katika soko la muziki alikiba  na anaamini kuwa watafanya kazi nzuri. Sister P ambae alikuwa akitamba sana kipindi cha nyuma na nyimbo zake kama Anakuja,Hey dj, na nyingine nyingi alizofanya na wasanii wenzie wakubwa  ameongea na studio za East Africa Radio na kusema kuwa anakaribia kuingia sokoni tena kwa kishindo kwa sababu amewamiss mashabiki zake lakini pia anasema kuwa kwa muda mrefu sana amekuwa akitamani kufanya kazi na Ali kiba kwa sababu yeye na Ali Kiba  sio wasanii bali ni wanamuziki hivyo wimbo wao lazima utakuwa mzuri sana. Kwa sasa nimejipanga vizuri ili kuweza kufanya vizuri mashambulizi ya muziki kwa sababu nina rudi tena katika muziki. Mwakani mwezi wa kwanzakuna ngoma nyingi sana ndani, nimefanya na mtayarishaji mpya katika muziki anaitwa Banny Music chini ya  Big Sound Studio.Lakini kiu yangu kubwa kabisa ni kufanya kazi na msanii Ali kiba kwani naamini kuwa itakuwa kazi nzuri sana na kubwa kwa sabau tutakuwa tumekutana wanamuziki sio wasanii. Alifunguka mwanadada huyo. Hata hivyo mwanadada huyo ambae alikuwa na muonekano wa kiume hapo awali kwa sasa anarudi kwa kishindo na kusema kuwa  atawashangaza watuw engi kwa sababu ana mpango wa kurudi kitofuati katika muziki na hata muonekano wake pia hautakuwa kama wa mwanzo.Mwanadada huyo anasema kuwa licha ya kukaa kimya kwa  muda mrefu katika game la muziki lakini atakapo rudi bado atajitahidi kurudi katika nafasi yake kwani anaamini kuwa anaweza sana. Wasanii wengi wa muziki wakongwe wa muziki waliokuwa wamekaa kimya kwa muda mrefu wameanza kurudi katika gam, hii ni kutokana kuwa muzikinwa sasa umekuwa na mafaniko yanayoonekana na umekuwa ni tofauti na ule wa kipindi cha mwanzo.

Maoni