DIWANI WA CHAMAZI AWATIA NDIMU VIJANA KWENYE MICHEZO

Mh diwani wa kati ya chamazi Ndg HEMEDI KARATA alitoa ahadi ya kuwasaidia vijana  asa kwenye michezo kwa kuwapatia vifaa vyote vya michezo ili vijana waipende michezo na waifanye michezo kama ajira,ahadi iyo alitoa wiki mbili zilizopia kwenye uzinduzi wa vikundi vya vijana (jogngg) vilivyo fanyika chamazi kwenye uwanja ulio pewa jina Karata. Leo  ijumaa tarehe 24/11/2017 toka kwa katibu hamasa na chipukizi kata ya chamazi Ndg NAJIM NURDIN NYANZA ametoa taarifa kwa vikundi vyote vya joggng vya UVCCM kwenye kata ya chamazi kujitokeza kwa wing siku ya jumapili tarehe 26/11/2017 kwenye uwanja wa karata ili kukabidhiwa vifaa ivyo vya michezo toka kwa Mh diwani uyo.

Nukuu " Katibu Hamasa na Chipukizi Kata ya Chamazi Ndg. *NAJIM NURDIN  NYANZA*anapenda kuwatangazia viongozi pamoja na wanachama wote wa UVCCM ambao Matawi yao yanamiliki *JOGGING* kuwa zoezi la kugawa jezi kwa jogging *TATU* za awali litakuwa tarehe 26/11/2017 saa moja na nusu asubuhi.

Kwa furaha kubwa anapenda kuwaambia viongozi na wanachama hao kuwa zoezi la manunuzi ya jezi hizo limekamilika kwa asilimia mia moja (100%).

Shukrani za pekee zimfikie Diwani wa Kata ya Chamazi Mh. *HEMEDI KARATA* kwa kuweza kufanikisha manunuzi ya *JEZI* hizo.

Kwa taarifa hiyo ndugu *NAJIM NURDIN NYANZA* anawasisitiza pia wana jogging wote kuhakikisha siku ya Jumapili wana amka mapema kwa ajili ya zoezi hilo.

Zoezi hilo litafanyika katika kiwanja cha mpira wa CHANDIMU cha *KWA KARATA*.

*RATIBA*

*Saa 12:15 Asubuhi*.

Jogging za Mbande Magengeni, Kisewe, Rufu na Mwembe Bamia zinakutana katika kiwanja cha mpira  *SONGAS*kwa ajili ya msafara wa pamoja kuelekea kwenye eneo la tukio.

*Saa 12:45 Asubuhi*.

Jogging za Mzambarauni, Kwa Mkongo, Dovya A, Dovya B zinakutana katika uwanja wa Mpira wa shule ya Msingi Chamazi kwa ajili ya kuzisubiri jogging zinazotoka uwanja wa mpira *SONGAS*.

*Saa 1:00 Asubuhi*

Kunywa uji kwa jogging zote katika kiwanja cha mpira cha *KWA KARATA*

*Saa 1:25 Asubuhi*

Zoezi la kuzindua jogging ya DOVYA A.

*Saa 1:30 Asubuhi*.

Zoezi la ugawaji jezi kwa jogging tatu litaanza rasmi.

Pia Ndg. *NAJIM NYANZA* anawaomba wana jogging wote zisizo za UVCCM kujitokeza katika tukio hilo ili kukuza udugu, umoja na mshikamano kwani UMOJA NA NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU.

Shime Shime wana UVCCM tujitokeze kwa wingi katika zoezi hilo

*IMETOLEWA NA*
*IDARA YA HAMASA NA CHIPUKIZI*
*UVCCM KATA YA CHAMAZI*
*24/12/2017*.

Maoni