YANGA WAPEWA SIKU 14 KUMLIPA KAKOLANYA WAKISHIDWA BASI

siku 14 viongozi wa klabu ya Yanga kumlipa mteja wake golikipa Beno Kakolanya  wakishidwa tu hatua zingine zitachukuliwa Kama Sheria na kanuni za usajili zinavyoelekeza hayo yamesema na meneja wa Kakolanya ndg Seleman Haroub.

"Ni kweli tunawadai Yanga fedha ya usajili iliyobaki,  Mara kadhaa tumekuwa tukiwakumbusha kwa njia ya mdomo tukiamini kwamba watashughulikia ila imekuwa ngumu hivyo tumewaandikia barua rasmi na kuwapa muda wa kulifanyia kazi "

"Ukiangalia kanuni za usajili tayari Yanga wamevunja mkataba na beno kwani makubaliano ya kutumalizia hiyo pesa yamepita na tumewavumilia,  na wakishidwa kumlipa kwa muda ambao tutakuwa tumewaelekeza tutakwenda Tff ili Kama vip mchezaji awe huru kabsa "

-Beno Kakolanya alijiunga na Yanga June 2016 akitokea Tz Prison na kusaini mkataba wa miaka miwili ambao unamalizika June mwakani katika kikosi cha Yanga Beno ameshidwa kuonyesha kiwango kumushawishi kocha kumpa namba katika kikosi cha kwanza msimu ulipita alikuwa anachuana na akina Ally Mustafa na Deo Munishi na alifanikiwa kucheza mechi za mwishoni wa msimu na msimu huu bado Beno  hajaichezea Yanga hata mechi moja ya ligi kuu Tanzania Bara baada ya usajili wa Mcameroon Youthe Rostand ambaye amekuwa chagua la kwanza mbele ya Benno Kakolanya na Ramadhan Kabwili.

Maoni