ZIJUE FAIDA ZA KIAFYA ZA KULALA BILA NGUO

Maishani, tunajikuta tunatakiwa kuvaa nguo tukiwa karibu kila sehemu, kwahiyo hamna sababu yoyote ya kung’ang’ania kuzivaa hata unapokwenda kulala. Mwanzo unaweza kuona ni jambo la ajabu sana kulala bila kuvaa chochote ila wataalamu wanasema kuwa hilo ni jambo lenye faida kubwa kiafya. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa kuhusu jambo hili “Sleep Survey” ni takriban asilimia 8 tu ndio hulala bila kuvaa chochote. Bila shaka watu wengi zaidi watakuwa wanajitupa kitandani bila kuvaa chochote baada ya kujua faida za kulala wakiwa watupu.
Zifuatazo ni baadhi tu ya faida zake:
Utapata usingizi mzuri zaidi
Japo nguo za kulalia (pajama) zinaweza kuonekana ni laini sana na zenye kuupa uhuru mwili wako, zinaweza kuwa chanzo cha kero na bughudha wakati umelala. Kwanza, pajama ukiongeza shuka au blanketi la kujifunika linaweza kuongeza joto la mwili hali inayoweza kukupa tabu kupata usingizi na kulala kwa starehe zaidi. Mwili unahitaji hali ya joto dogo sana (baridi kiasi) ili uweze kupata usingizi mzuri – lakini kwa nguo zote hizo unazofaa, mwili wenyewe unaweza ukaupa tabu kubwa kugundua kwamba muda wa kulala umeshawadia.
Unapovua nguo zote, ngozi kiasili itapoa haraka zaidi na kuufanya mwili wote upumzike mapema zaidi tangu upande kitandani au sehemu yoyote ambayo unalala, lakini kuvaa pajama kunafanya mwili ushindwe kufanya unachotakiwa ili kukusaidia ili upate usingizi mapema.
Unaupa mwili nafasi ya kupumua na kukuepusha na maambukizi ya bakteria
Kwakuwa tunavaa nguo muda mrefu zaidi kwa siku, hatupati nafasi ya kuupa mwili fursa ya “kupata hewa,” hasa kwa wanawake. Kuvaa chupi wakati wa kulala unafanya vijidudu vya bakteria na fangasi wabaki ndani yako na kuwapa mazingira mazuri zaidi ya kundelea kukua na kuzaliana kirahisi. Watu wanapolala bila nguo, kitabibu ni kwamba wanapunguza uwezekano wa kupata maambukizi yanayotokana na bakteria wanaonyemelea sehemu zenye unyevu na hivyo kuufanya mwili kujikausha na kukuacha salama zaidi. Pia, utajisikia vizuri zaidi mwili wako unapopata hewa bila kuzuiwa na nguo yoyote.
Kulala bila nguo kando ya mpenzi wako kunapunguza msongo wa mawazo
Wengi wanajua kwamba kushikwashikwa na mpenzi wako au kukumbatiwa kunaimarisha afya kwa namna nyingi sana, lakini mnapoamua kulala bila kuvaa nguo yoyoye itaongeza faida hizo kwa kiwango ambacho huwezi kutegemea kabisa. Kupata hisia za mgusano wa “ngozi kwa ngozi” na mpenzi wako uliyelala naye kutakusaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza msongo wa mawazo, kusaidia kupunguza shinikizo la juu la damu na kuufanya mwili uwe huru na kustarehe zaidi – bila kusahau kwamba mnapolala bila kuvaa nguo yoyote kutawafanya wewe na mpenzi wako muwe na furaha zaidi hivyo kuwa na afya bora zaidi na kupelekea kila mmoja kuwa nafuraha zaidi mnapojamiiana.
Utajiona upo karibu zaidi na mpenzi wako
Si jambo la kushangaza kuona kwamba utafiti uliofanywa mwaka 2014 kwa wanandoa 1,000 nchini Uingereza ulibainisha kuwa wanandoa wenye mazoea ya kulala bila nguo walikuwa na ndoa yenye furaha zaidi ya wale waliokuwa wanalala wakiwa wamevaa nguo. Kwa usahihi zaidi, asilimia 57 ya watu waliosema walikuwa wanalala bila kuvaa nguo waliripoti kuwa wanatoshelezwa na uhusiano wao wakati ni asilimia 48 ya wanaolala na pajama au nguo nyingine wakati wa kulala ndio walisema kuwa wanatosheka kwenye uhusiano wao. Kwa matokeo ya aina hii, bila shaka inaweza kuonekana kuwa ni salama na vizuri zaidi kulala bila kuvaa nguo kwakuwa itakufanya uwe karibu zaidi na mpenzi wako na kufanya uhusiano wenu uwe mzuri zaidi.
Kulala bila kuvaa nguo inasaidia kupunguza uzito wa mwili
Unapokosa usingizi wa kutosha kiwango cha msongo wa mawazo kinaongezeka na kukufanya upate hamu kubwa ya kula vyakula visivyo na faida yoyote kwenye afya ya mwili wako. Wakati unapolala, homoni zako za kuufanya mwili ukue zinazoongezeka huku homoni zinazoongeza msongo wa mawazo (cortisol ) zinapungua. Hii ni njia ya kiasili ya kuufanya mwili kubaki sawa na kukufanya usipate msongo wa mawazo. Lakini kutopata usingizi wa kutosha kunafanya kemikali hizi za kuufanya mwili uwe sawa zishindwe kuwa katika uwiano mzuri.
Kulala bila nguo kunafanua mwili wako upumue vizuri zaidi jambo litalokusaidia ulale vizuri kwa muda mrefu zaidi.
Asubuhi unapoamka, homoni zinazopandisha msongo wa mawazo huwa zinaongezeka tena ili kutupatia nguvu na uwezo wa kufanya kazi. Hata hivyo, kama hatutaupa mwili fursa ya kupunguza homoni hizi zinazoongeza msongo wa mawazo, ni rahisi kujikuta tuanakimbilia vitu tutavyoona vitasaidia kujisikia vizuri kama vyakula na vilevi.

Maoni