ASANTE KWASI, DOMINGOS WATIA SAINI KUITUMIKIA SIMBA SC

Pichani ni wachezaji wapya wa Simba Antonio Domingos na Asante Kwasi wakisaini mikataba Jana usiku kwa ajili ya kuitumikia Simba.

Simba imemsajili Kwasi kwa ajili ya kuziba pengo la Method Mwanjali aliyeachwa siku chache zilizopita.
Imeelezwa kuwa Antonio Domingos amesajiliwa kwa ajili ya kuziba nafasi ya Laudit Mavugo aliye kwenye mazungumzo na klabu za Kenya na Oman kwa ajili ya kusajiliwa huko.

Taarifa kutoka ndani ya Simba zinadai wachezaji hao wataungana na wenzao Jumatatu kwa ajili ya mazoezi ya kujiandaa na michezo ijayo ya ligi Kuu na ile ya kombe la mapinduzi.


Maoni