Azam Yaifanyia Kufuru Villa Squad Yaitandika Kipigo Cha Paka Mwizi..

Klabu ya Azam imeibugiza klabu ya Villa Squad jumla ya goli 7-1 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa jioni ya leo December 16.2017 katika uqanja wa Azam Complex.
Katika mchezo huo Azam walianza kupachika goli la kwanza mnamo dakika ya 6 kupitia kwa Joseph Mahundi kabla ya dakika ya 13 Mahundi tena kuipatia Azam bao la pili.
Dakika ya 26 Yahya Zayd aliongeza bao la tatu kwa Azam baada ya kuitumia vyema uzembe wa mabeki wa timu ya Villa Squad bao lilidumu hadi kumalizika kwa kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili kilirejea kwa nyota wake aliesajiliwa msimu huu”Bernard Arthur” kuifungia Azam goli la nne na kuongeza goli la tano mnamo dakika ya 59.
Dakika ya 62 Bruce Kangwa aiongezea Azam goli la 6 kabla ya Villa Squad kufunga goli la kufutia machozi mnamo dakika 73 na hatimae Wazir Junior kukamilisha karamu ya magoli kwa kuifungia Azam goli la 7.
Hadi kipenga cha mwamuzi kinapulizwa kuashiria kutamatika kwa mtanange huo Azam waibuka kifua mbele kwa mabao 7-1 ya Villa Squad.

Maoni