BALL TALENT (KWA MSOMA) MABINGWA WA MKALIPA CHRISTMASS CUP

MASHINDANO ya ligi ya kombe la Mkalipa Christmass Cup,yamefikia tamati kwa timu ya soka ya Ball Talent kuwa mabingwa wa kombe hilo  baada ya kuifunga timu ya Mchaka mchaka FC kwa jumla ya magoli 3-0.
Ligi hiyo iliyoanza kuchezwa Dec, 22 mwaka huu kwa makundi mawili yaliyokuwa yakitumia kiwanja cha Kwa Gogo ilizishirikisha jumla ya timu nne za eneo ilo ambazo ni pamoja na KeyTeam, Ball Talent Fc (Kwa Msoma), Buti Kubwa, na Mchaka mchaka Fc (vululumparara).

Kwa upande wake muandaaji wa kombe hilo ambaye pia ni Mwenyekit wa UVCCM kata ya chamazi,Nasri Mkalipa aliyataja baadhi ya malengo ya michezo hiyo kuwa ni kuhakikisha wanakuza pamoja na kuvitangaza vipaji vya vijana hao kupitia sekta ya michezo.

Maoni