CHAMAZI YAPATA MWAKILISHI MAFUNZO YA UONGOZI YALIO ANDALIWA NA TAHLISO


Mjumbe wa mkutano mkuu wa wilaya akitokea kata ya chamazi ambaye pia ni katibu wa hamasa na chipukizi wa tawi la Mfenesini Ndg Neema Pius Divalina Leo tarehe 13-12-2017 ameshiriki semina ya siku mbili ya uongozi ambayo imeandaliwa  na shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu nchini (Tanzania Higher Learning Institution Students organization) kwa kifupi TAHLISO.

Akizungumza kwa njia ya simu diva alisema "Tahliso wameandaa workshop kwa wasomi viongoz wa serikali za wanafunz vyuo rais,makam wa rais, mawazir na wabunge na waliomaliza vyuo nchi nzima lengo ni kuwapa chachu ya uongozi katik nyanja ya vyuo na mafunzo hayo yatakuwa endelevu ili Kumjenga kiongoz Katika kufanya maamuzi ya kimkakati,kuwa na sifa binafsi ambazo zinamfaya kiongozi kuwa bora hususan katika mavazi,kuongea, kutembea na hata nidham vilevile mafunzo hayo yamelenga katika Uongozi bora katika kutumika na changamoto zinazokabili uongozi wa ki Africa hivyo nitatumia mafunzo Haya pia kuelekeza viongozi wenzangu ili wote kwa pamoja tuwe viongozi bora si tu kichama Bali na taifa kwa jumla" Aliongeza diva.

Mafunzo hayo yanakufunzwa na waziri ofisi ya makamu raisi  mazingira Mh January Makamba na yatakuwa ya siku mbili kwa maana leo Dec 13 na kesho Dec 14.

*Imetolewa na*
*Idara ya hamasa na chipukizi*
*UVCCM-CHAMAZI*

Maoni