HASARA NA MADHARA YA KUTOFANYA MAZOEZI

Kutofanyara mazoezi  kuna hasara na madhara mengi. Baadhi yake ni
1. Mwili huwa mzito, hukosa kuwa imara na huwa sio uliojiandaa kukabiliana na dharura
2. Kinga ya mwili hushindwa kuwa imara zaidi na utapata hata magonjwa na maambukizi madogo madogo
3. Uzito wa mwili kuwa mkubwa (obesity) na hatari kwa afya yako
4. Mwili unakuwa katika hatari ya kupata magonjwa yasiyoambukizwa kama vile kisukari, presha, uzito mkubwa uliopitiliza (obesity), msongo na magonjwa ya moyo na mfumo wa damu
5. Kuwa na manyama uzembe, kitambi kwa akina baba na tumbo kubwa kwa akina mama
6. Mwili haujengeki vizuri na mtu huweza kukosa umbo zuri
7. Kuwa na mrundikano wa mafuta mwilini na kwenye mishipa ya damu – HATARI SANA!
USHAURI
Mazoezi huberesha afya, huzuia magonjwa na hata kupunguza uwezekano wa kufa mapema. Fanya mazoezi ili uweze kuishi muda mrefu. Sio lazima ufanye mazoezi magumu, ya gharama au mbali na ulipo – Anza na yale utakayoyamudu kwa urahisi. Unaweza ukaamua kutembea au kukimbia umbali fulani kila siku, ruka kamba, nyanyua vitu vizito nk kulingana na nafasi yako.
Boresha maisha yako. Refusha maisha yako. Fanya mazoezi!

Maoni