JOKATE NIPO TAYALI KUFUNGUA MASHINDANO YA REDE CUP CHAMAZI

Leo Jumanne Dember 05 2017 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Chamazi Ndg. Nasri Bakari Mkaripa amefanya mazungumzo na Kaimu Katibu wa hamasa na chipukizi UVCCM Taifa Ndg. Jokate Mwegelo.

Mazungumzo hayo yamefanyika ofisini kwa Ndg. Jokate Makao Makuu ya UVCCM Upanga jijini Dar es Salaam.

Sambamba na mambo mengine Ndg. Mkaripa alimtaka Ndg. Jokate kuja Kata ya Chamazi na kujionea vipaji vilivyopo Katika Kata hiyo.

Nukuu _"Kata ya Chamazi kuna vipaji vingi vya michezo mbalimbali kwa hiyo kama mdau nakuomba usapoti michezo hiyo, kwa sasa tumeanza na REDE ambapo awamu ya kwanza imemalizika Jumapili na Timu ya Wazalendo kuwa washindi"_ alisema Mkaripa..

_"Mwezi wa Kwanza tunatarajia ligi hiyo kuanza kwa ngazi ya KATA ambapo timu kutoka matawi 13 ya Kata ya Chamazi zitashiriki ligi hiyo, kwa hiyo nichukue fursa hii kuomba sapoti yako na hatimaye kuendeleza michezo Kata ya Chamazi"_ alisema Mkaripa.

Akizungumza wakati wa kikao hicho Ndg. Jokate alikubali kuwa mdau namba moja wa michezo Kata ya Chamazi na kuahidi kuwa nao bega kwa bega katika michezo kwani michezo ni ajira.

_"Mara nyingi huwa nawafatilia mitandaoni na naona jitihada zenu za kuendeleza michezo, naahidi kuwa nanyi bega kwa bega katika michezo ya aina yoyote na niwaahidi kuwa Mungu akipenda nitafungua ligi ya REDE YA KATA yenu"_ alisema Jokate.

_"Pia nawaasa Kata zingine ziige mfano wa Kata ya Chamazi wa kuendeleza vipaji vya michezo kwani michezo ni ajira"_ alisema Jokate.

Maoni