KISEWE QUEENS WATAMBA KUWAFUNGA MZAMBARAUNI KWAO.

Kuelekea kwenye mchezo wa kirafiki wa Rede utakao zikutanisha team ya KISEWE QUEENS na MZAMBARAUNI QUEENS siku ya jumapili kwenye uwanja wa mzambarauni majira ya saa 10 jioni.
Kwa nyakati tofauti ShabaniRapwiBlogsport.com imepata fursa ya kuongea na baadh ya wachezaji wa KISEWE QUEENS kuelezea maandalizi yao ya mchezo uwo.
                        
 "Tina"

"Timu iko vizuri na tumejipanga vizuri kuwapa dozi ya kutosha kila mmoja ana molali ya mchezo uwo, kwa wiki nzima sasa tumekuwa tukifanya mazoezi asubuh na jioni kujianda na mchezo uwo wa jpili, Mzambarauni ni timu ya kawaida sana japo walishawai kutufunga goal 3 kwa 0,Lakini nataka kuwambia wanakisewe wasiwe na presha tumejipanga kwa ajiri ya ushindi tu iyo jumapili"

SR..   swali  kwa tina Unazungumziaje swala la uchawi kwenye michezo na unaamini kuwa uchawi upo? 

Tina "Ndio maamini uchawi upo japo sijawai fanya uchawi ata siku moja naamini mazoezi na kujituma kwangu uwanjani ndio mafanikio yangu,pia mi nawamini sana mungu nasio imani izo"

SR..  Nini ushauri wako kwa team sasa zinazo amini uchawi?

Tina "Waache sio vizuri na haipendezi michezo ni furaha"

Team Captain 
"Kwanza naombea iyo jumapili ifike haraka maana Mzambarauni nilikuwa nawataka sana ndio maana nafanya mazoezi kwa bidii,ni razima tutawafunga tu"
SR.. swali kitu ngani kinakufanya ujiamini sana?

Captain "Kwa sababu tumejianda vya kutosha, juzi tu tumetoka kuchezaa na Kiponza Queens na tumewafunga goal 3 kwa 0"

SR.. swali ni mchazaji ngan unae mwofia kwenye team pinzani?

Captain "Hakuna ninae mwofia wote ni wakawaida tu,sisi tupo vizuri sana. 


Maoni