"Jukumu la kuijenga chamazi ni letu wenyewe wanachamazi" - Mkaripa

 Mwenyekiti wa umoja wa UVCCM kata ya chamazi Ndg Nasri Mkaripa amesema "Ni muhimu kwa kila mwanachamazi asa vijana kujitoa kuijenga na kuitangaza chamazi kwenye kila nyanja,ili chamazi iwe mfano wa kuingwa kwenye kata zingne " ameyasema ayo kupitia kwenye tafrija fupi ya mapokezi yake siku ya jana Dec 12 akitokea Dodoma kwenye mkutano wa tisa wa chama cha mapinduzi taifa
Pia Ndg Mkaripa amesema "Katika wilaya ya temeke kata bora chamazi ni moja wapo,maana nimekutana na viongozi wengi wa chama cha mapinduzi wakinipongeza kwa juhudi za wanachamazi,hii inadhilisha wazi kuwa tunacho kifanya kinaonekana ivyo tuzidishe zaid ya hapa,mimi binafsi nikishirikiana na viongozi wenzangu tutakikisha tunaipigania chamazi kwenye maendeleo kwa nguvu zetu zote ivyo wanachamazi tushirikiane na tushikamane, maendeleo yanaitaji ushirikiano wa kila mmoja wetu,bira ya kuangalia rangi,dini,kabila wala jinsia". amesema Mkaripa. 


Baada ya kuyasema ayo pia alipongeza kamati ya michezo na burudani kwa kufanya kazi nzuri  kwenye michezo na burudani kwa ujumla ndani ya kata ya chamazi rakini pia Mkaripa halitoa ovyo kwa viongozi wa kamati mbalimbali wasio wajibika na amewambia kama wameshindwa wajiudhuru wenyewe kwenye nafasi izo na wakae watu wanao chapa kazi na kujituma.

Maoni