LIGI KUU TANZANIA BARA SASA KUCHEZWA MIDA YA SAA 8 MCHANA

Baada ya kusimama kupisha mashindano ya Cecafa Chalenji ligi kuu ya Vodacom itaendelea tena mwishoni mwa mwezi huu huku baadhi ya mechi zikipangwa kuanza saa 8 mchana.
Sababu ya mechi hizo kupangwa muda huo ni kutokana na michezo mingi kutakiwa kuonyeshwa moja kwa moja (live) ili kuondoa hujuma ambazo zinaepukika. Afisa Mtendaji wa bodi ya ligi (TPLB) Boniface Wambura amesema utaratibu huo utapunguza malalamiko kutoka Kwa klabu juu ya waamuzi pia litakuwa ni jambo zuri kwa wadhamini wa ligi, klabu pamoja na Shirikisho lenyewe.
"Baada ya ligi kusimama kupisha michuano ya Chalenji itaendelea tena Disemba 29 na safari hii kuna baadhi ya mechi zitakuwa zinaanza saa 8 mchana kwakua tunataka ziwe zinarushwa moja kwa moja na Azam TV. "Tumeamua kufanya hivi ili kupunguza malalamiko juu ya waamuzi kwakua mechi nyingi zitakuwa live na zile zitakazofanyika kwenye uwanja wa Azam Complex zitapigwa saa 1 usiku," alisema Wambura.
Mechi za raundi ya 12 ni December 29; Azam vs Stand United (saa 1 usiku)
December 30; Lipuli vs Tanzania Prisons (saa 8 mchana)
Mtibwa Sugar vs Majimaji (saa 10 jioni)
Ndanda vs Simba (saa 10 jioni)
December 31; Njombe Mji vs Singida United (saa 8 mchana)
Mbao vs Yanga (saa 10 jioni)
January 1; Mbeya City vs Kagera Sugar (saa 10 jioni)
Mwadui vs Ruvu Shooting (saa 10 jioni).
Hata hivyo baada ya mzunguko huo ligi itasimama tena kupisha michuano ya Mapinduzi itakayofanyika visiwani Zanzibar kuanzia mwishoni mwa mwezi huu.

Maoni