MAONI YA WANANCH JUU YA MASHINDANO YA REDE CUP 2017 YALIO FANYIKA CHAMAZI

Wananch wengi wamekuwa na maoni mbalimbali baada ya kukamilika mashindano ya Rede Cup 2017, Dec 03 na team ya Wazalendo Queens kuibuka na ubingwa wa michuano iyo kwa mwaka huu 2017.

shabanirapwiblogsport.com tumefanikiwa kufanya maojiano na baadh ya wananch walio kuwa wanafatilia mashindano aya.

Rajabu Salehe - "Kwanza nawapongeza waandaji wa mashindano yale kiukweli wamejitaidi sana na nawapongeza sana"

Amina Juma - "Mimi kama mwanamke nimefurahi kuona ligi ya rede maana nilipo kuwa naishi mwanzo sikuwai kuona ligi kama hii kulikuwa tu na mabonanza rakini wanawake hatukupewa nafasi sana waliokuwa wanapewa nafasi ni wanaume kucheza mpira wa miguu,natamani ligi itakapo anzishwa tena na mimi niwe mchezaji"

Saimoni Simenya - "Kuwepo kwa mashindano aya ya rede cup hapa chamazi ni jambo zuri la kutia hamasa dada zetu na wanawake kwa ujumla kwenye michezo,kuna siku nakumbuka nilikuja kuangalia mech hapa nilifurahi kuona mama mjamzito nae anacheza kiukweli nilifarijika sana rkn ombi langu kwa waandaji waongeze team nying zaid ili ushindani uwe mkubwa,ayo ndo maoni yangu"

Mama Hasani - "Mashindano ya rede kwanza yametunganisha wanawake na kutuweka pamoja na kutufanya tuwe sote wamoja bira kujali rangi,kabila wala dini,nawapongeza wazalendo kwa kuwa mabingwa"

Khalima Mohamedi - "Maoni yangu waandaji watafute  team moja ya rede itakayo wakilisha  kata nzima ya chamazi kupitia team zote zilizo shiriki mashindano aya ya rede cup kwa mwaka huu 2017 "

shabanirapwiblogsport.com tutatoa shukran kwa wote mlio tupa ushirikiano.

Maoni