MGAMBO MARUFUKU KUONEKANA KATIKA KITUO CHA POLISI KATA YA CHAMAZI


Leo Ijumaa 22 Desemba 2017 nimefanya kikao kidogo na Polisi Kata ya Chamazi Sgt. Joseph Chacha katika Ofisi yake Kituo cha polisi Chamazi.

Kikao hiko kilikuwa na lengo la kujua mustakabali wa Vijana kutokana na lawama kukamatwa hovyo na mgambo waliopo katika ofisi hiyo.

Malalamiko hayo ya vijana kutoka katika Mitaa yote ya Chamazi yamenifikia katika nyakati tofauti.

Kesi nyingi za vijana zimekuja kwangu nami kama kiongozi wao nikasema Nina wajibu wa kulifatilia hili na kujua mustakabali wake.

Akizungumza wakati wa mazungumzo hayo Sgt. Chacha alisema hata yeye kero hizo zimemfikia na ameahidi kesho Jumamosi 23 Desemba 2017 ndio itakuwa siku ya mwisho ya mgambo hao kuonekana katika kituo hicho.

Ikitokea mtu yoyote amekamatwa na  mgambo asisite kunipigia simu kwa Mwenyekiti  Nasri Mkaripa kwa  namba yake 0713 311 300 au 0620 881 532.

Mkaripa amesema Lengo ni kumuunga mkono RAIS MAGUFULI kwa kutokomeza  RUSHWA katika Kata yangu ya CHAMAZI.

"Nikisikia kijana umekamatwa na Mgambo na kwa uoga ukampa pesa nitakupeleka katika vyombo vya sheria kwani mtoa rushwa na mpokea rushwa wote ni sawa" amesema Mkaripa

Maoni