MKALIPA ASHEREHEKEA BOXING DAY NA WATOTO YATIMA CHAMAZI

Na Shabani Rapwi

Chamazi, Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Chamazi Ndg. Nasri Mkalipa amesherehekea siku ya pili ya sikukuu ya Christmas's (Boxing Day) kwa kuwatembelea na kufurahi na watoto wanaoishi katika mazingira magumu (yatima)

Ziara hiyo ya kuwatembelea na kufurahi na watoto hao imefanyika leo 26 Desemba 2017 katika kituo wanacholelewa watoto hao kinachojulikana kwa jina la Yatima Trust Group Fund kilichopo Chamazi jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa ghafla hiyo iliyohusisha michezo ya aina mbalimbali sambamba na kupata chakula cha pamoja Ndg. Mkalipa aliwata watanzania kuwathamini watoto wanoishi kwenye mazingira magumu kwa kuwatembelea mara kwa Mara na kuwafariji.

"Leo nimeamua sikukuu yangu iishe kwa kujumuika na watoto hawa wanaishi katika mazingira magumu, kuwa hapa sio kwamba wamependa hapana nao walitamani kuishi na wazazi wao huku wakideka" alisema Mkalipa.

"Lakini kwa bahati mbaya hilo kwao halipo wamekuwa wakiishi pasipo na wazazi kwa hiyo nichukue nafasi hii kuwaasa watanzania wenzangu kutumia muda wetu vizuri kwa kuwatembelea na kuwapa faraja watoto hawa na kwa walionacho hata kidogo tukitumie kwa kuwaletea mahitaji madogomadogo watoto wetu hawa" alisema Mkalipa.

Pia Mkalipa aliwataka vijana hao waliofikisha umri wa kusoma na waliopo mashuleni wahakikishe wanasoma kwa bidii kwani elimu ndio mkombozi wa maisha.
Mwenyekiti hapa hakiwa anawasili kwenye kituo iko cha watoto yatima. 
Hapa Mwenyekiti Nasri Mkalipa akisalimiana na mmoja ya wadau alio kutana nao kwenye kituo iko. 


Mwenyekiti akimtangaza mshindi wa kucheza singeli uku akitoa zawadi kwa watoto hao.  

Maoni