MKALIPA - CHAMAZI HATUPO TAYALI KUTUMIKA KWA MASLAHI YA MTU BINAFS

Vijana wametakiwa kutokubali kutumiwa vibaya na baadhi ya viongoz  kwa maslahi ya watu wachache huku hao wanaowatumia wanasonga mbele kimaendeleo na wao wanazidi kurudi nyuma.

Rai hiyo imetolewa leo Dec 19 na Mwenyekiti UVCCM chamazi ,Nasri Mkalipa akiongea na shabanirapwiblogsport.com

alisema kuna baadhi ya viongozi wanawatumia vijana kwa maslahi yao binafsi  "Chamazi tumeamua kutotumika kwa maslahi ya mtu binafsi bali tutatumika kwa ajili ya chama tu,hatutaki pesa ya mtu,tunataka maendeleo ya vijana katika sekta zote na maendeleo hayo yanakuja kwa kushirikiana pamoja" amesema Mkaripa

Pia ndg Mkalipa akaendelea kwa kusema "VIJANA JEURI YA CHAMA alafu wapiga kura wengi ni vijana sasa kwa nini tusijipe thamani? badala yake wanatutegea na kusubiri uchaguzi ndio wanatuletea jezi,mipira na kuanzisha maligi kibao,waige mfano wa Rais wetu mpendwa Mh. John Pombe Magufuli,Mabadiliko yameanza sasa UVCCM chamazi tunajithamini na tunaomba tuheshimiwe"

Mkalipa pia alitoa Pongezi kwa Mh Diwani wa kata ya chamazi Ndg Hemedi Karata na Mwenyekiti  wa Serikali ya Mtaa wa Kisewe Ndg Mwalile kwa kuwajali na kuwathamini vijana kwenye sekta ya Michezo.

Maoni