MKALIPA CHRISTMASS CUP KUANZA KURINDIMA KESHO CHAMAZI.

Kuelekea siku ya kumbukizi ya kuzaliwa Yesu Kristo, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Chamazi Ndg. NASRI MKALIPA ameanzisha michuano ya siku tatu kuelekea maadhimisho ya sikukuu hiyo.

Ligi hiyo fupi inahusisha timu nne za mpira wa miguu (CHANDIMU) kutoka katika Mtaa wa KWA MSOMA.

Timu hizo ni Buti kubwa,KeyTam, Vululumparara na Ball Tallent.

Akizungumza baada ya kuchezesha  droo ya timu zinazoshiriki ligi hiyo Ndg. Mkalipa alisema ameanzisha ligi hiyo ili kuwawezesha vijana kufurahi kuelekea siku hiyo muhimu kwa waumini wa dini ya Kikristo dunia nzima.

_"Tunaelekea katika siku muhimu kwa wakristo dunia nzima, nami katika kuazimisha siku hiyo nimeamua kuanzisha ligi hii ili kuleta hamasa kwa vijana na hatimaye kuikaribisha vyema siku hiyo"_ alisema Mkalipa.

_"Nawathamini sana vijana kwani ndio tegemeo la Taifa, sasa kupitia ligi hii Nina uhakika upendo wetu utakuwa mkubwa na pia mtakuza vipaji vyenu, niwahidi tu kuwa tutakuwa na utaratibu wa kuwa na ligi kama hizi kila inapokaribia sikukuu yoyote ya Dini au ya Kitaifa ili kuikaribisha siku hiyo"_ alisema Mkalipa.

Wakati huo huo droo ya ligi hiyo imechezeshwa leo na ratiba ya ligi hiyo itakayochezwa katika Kiwanja cha KWA GOGO ni kama ifuatavyo.

Kesho Ijumaa 22/12/2017 KUNDI A

Vululumparara VS KeyTam.

Kesho Kutwa Jumamosi KUNDI B 23/12/2017

Buti Kubwa VS Ball Talent.

Jumapili 24/12/2017

Fainali

Mshindi wa kundi A na mshindi wa kundi B.

Karibuni Sanaaa.

*Imetolewa na*
*Kamati ya Ligi*
*Mkalipa Christmass Cup*.

Maoni