Mkaripa Atoa Neno Baada Ya Zoezi La Usafi Kukamilika

Mwenyekiti Wa Uvccm Kata ya Chamazi Ndg Nasri Mkaripa na Katibu Hamasa Na Chipukizi Ndg Najim Nyanza leo wameongoza zoezi la usafi kata eneo la Kiponza Jijini Dar es salaam ikiwa ni utekelezaji wa Agizo la Rais John Magufuli katika kupambana na maradhi ya Mlipuko yanayotokana na uchafu.

Katika Mitaa mbalimbali ya eneo ilo viongozi hao na wananch pamoja na vikundi vya vijana maarufu kama (JOG) wamejitokeza kufanya usafi wa mazingira ambapo hata hivyo mwitikio wa wananch haukuwa mkubwa sana ni wananch wachache sana ndio walio jitokeza katika zoezi ilo.

Mkaripa alipata fursa ya kuongea na vijana na kuwambia "vijana tujitume sisi ni nguvu kazi ya taifa japo wananch hawakutoa ushirikiano mkubwa sana hapa msijisikie vibaya na msikate tamaa,tuzidi kujitolea na kuamasika kwenye mazoezi kama aya naimani zoezi limeenda vzuri kama tulivyo tarajia" amesema Mkaripa

Pia Mkaripa ametoa ovyo kali kwa kijana yeyote atakae kamatwa na mgambo na akatoa urushwa basi atampa adhabu kali "Mtu akija kukukamata ana budi kukuonesha kitambulisho kwamba mimi polisi kile kitambulisho ndicho kitakacho kufanya wewe umwamini na kwenda kituoni, kwaiyo akija mgambo kukamata kata,usikamatwe na mgambo nipigie kwenye namba yangu 0713311300 au 0620881532 ombi langu ewe kijana usitoe rushwa kwa maana ukikamatwa na mgambo na ukatoa rushwa kuna usemi unasema Mtoa rushwa na Mpokea rushwa wote ni sawa,mimi kama kiongozi wako nitakuukumu kwa kutoa iyo rushwa" amesema Mkaripa.

kijana wa club ya jog akikata nyasi
Hawa ni baadhi ya vijana walipo kuwa kwenye zoezi la usafi Kiponza. 
Zoezi la usafi hapa likiwa linaendelea uyo ni moja ya wananch walio jitokeza akiwa ana Lima. 


Picha na shabani rapwi

Maoni