MUHUNZI - "KUFUNGWA SI SABABU YA KUKOSA FURAHA"

Ni kauli yake Muhunzi meneja wa team ya mzambarauni amesema  Nukuu"Kufungwa si sababu ya kukosa furaha tuajipongeza kwa kuonyesha mchezo mzuri  na kwa nidhamu ya hali ya juu  ,nimejiridhisha pasi  na shaka kuwa tunatakiwa kuongeza bidii ktk mazoezini ,na ndio nikaona hata kama hatujashinda basi tuakaoshe kidogo kula Italian pizza".

ameyasema ayo baada ya team yake kukubali kichapo cha goal 3-0 toka kwa Kisewe Queens.

Pia Muhunzi amesisitiza watu kutokuwa na majungu pindi wanapo fungwa "Kufungwa ni sehemu ya mchezo nawapongeza kwa ushindi mmcheza vizuri ,mimi huwa sina majungu kama nimefungwa sina ulalamishi hata kama kuna mapungufu madogo madogo ni ya kibinadamu" kisha  akamalizia kwa kutoa ushauri "Ninachowashauri tuwe na uzalendo wa kukubali matokeo yatakayotokea mchezoni" amesema Muhunzi.

Na hii iwe mfano kwa team na viongozi wengne kukubari matokeo nasio kulalamika na kutoa lugha chafu za matusi. 

Maoni